Wakati Mhimili wa Mahakama unatoa huduma muhimu, zinazosimamiwa kikatiba kwa umma ambazo zinahitaji shughuli kuendelea wakati wa janga la COVID-19, tunachukua kila hatua inayowezekana kupunguza hatari. Tunaendelea kufanya mabadiliko ambayo yatahakikisha ufikivu wa mahakama huku tukilinda afya na usalama wa wafanyikazi wa mahakama na umma. Tumeongeza mwitiko wa Mhimili wa Mahakama kwenye COVID-19 kwani hitaji la kutotangamana limekuwa muhimu zaidi.
TAFADHALI SOMA MAAGIZO YOTE KATIKA KIPENDELE HIKI
ZUIO LA KUINGIA MAJENGO YA MAHAKAMA (PDF inayopakulika hapa)
Hakuna mtu ataruhusiwa kuingia au kubaki ndani ya jengo la Mahakama ya Haki ya Kentucky isipokuwa akiwa amevaa vikinga uso kama vile barakoa, skafu, bandana au kitambaa kingine ambacho kinaziba pua na mdomo.
Ikiwa mtu hana kikinga uso kinachofaa na shughuli yake haiwezi kukamilishwa akiwa mbali, atapewa kikinga uso.
Zaidi ya hayo, watu hawataruhusiwa kuingia jengo ikiwa:
- Dalili zozote za COVID-19, ikiwamo kukohoa, pumzi kubana au kupumua kwa shida, homa, baridi, uchovu, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa, kichefuchefu, kutokwa kamasi puani, kichefuchefu au kutapika, kuharisha, maumivu ya koo kutohisi ladha au harufu.
- Umeambiwa ukae karantini binafsi na daktari, hospitali au shirika la afya lolote.
- Umegundulika kuwa na COVID-19 ndani ya siku 14 zilizopita au ulikaribiana na mtu yeyote ambaye amegundulika kuwa na COVID-19 ndani ya siku 14 zilizopita.
MIPAKA YA HUDUMA ZA ANA KWA ANA (PDF inayopakulika hapa)
Wanaoruhusiwa tu kuingia katika majengo ya mahakama ni:
- Mawakili, wahusika, mashahidi, majaji, watetezi wa unyanyasaji wa majumbani, na watu waliopangwa au walioidhinishwa na jaji kufika katika usikilizaji wa mashauri ya ana kwa ana.
- Watu wanaotafuta amri za dharura za ulinzi, amri za ulinzi wa kati ya mtu na mtu, amri za dharura za malezi, amri za sheria ya Casey na ahadi zisizo za hiari.
- Watu wanaohudhuria mauzo ya mahakama.
- Watu ambao wanataka kupata mafaili halisi za mashauri au kituo cha kupata taarifa za kielektroniki na wameweka miadi na kalani wa mahakama.
- Watu ambao wameweka miadi na karani wa mahakama kwa ajili ya huduma za leseni ya udereva. Kumbuka: Leseni za udereva ambazo zimeisha kati ya Machi 1-Sept. 30, 2020, lazima zihuwishwe kwa mbali.
- Watu ambao wanafika kwa ajili ya vipimo vya dawa za kulevya vilivyopangwa.
Mashtaka yote lazima yatumwe kwa posta, kupitia mtandao (eFile) au yawasilishwe kama kawaida kwa kutumia sanduku la kukusanyia lililo nje ya jengo la mahakama.
Malipo ya gharama za mahakama, faini, ada na fidia yanaweza kulipwa kwa hawala ya fedha inayotumwa kwa karani wa mahakama, au kwa fedha taslimu au kwa kadi ya benki kwa kumpigia simu karani wa mahakama.
Malipo ya kabla ya hukumu yanaweza kulipwa kwenye mtandao kupitia ePay.
Watu wanaotuma dhamana wanapaswa kuwasiliana na karani wa mahakama kwa maelekezo zaidi.
Ili kuomba nafasi ya umma kuingia kwenye masikizo, wasiliana na karani wa mahakama kwa ajili ya mwongozo.
Watu wasiokidhi vigezo vya kuingia katika jengo la mahakama wanapaswa kuwasiliana na karani wa mahakama ili kupanga upya ratiba, kuhudhuria kwa mbali, au vinginevyo ili kukamilisha shughuli zake za mahakama.
Angalia kipengele cha Fomu, Machapisho, na Nyenzo hapo chini kwa kadi ya “NINAZUNGUMZA KISWAHILI” unaweza kumwonyesha karani ili kuomba mkalimani.
MIPAKA YA POCHI NA MABEGI (PDF inayopakulika hapa)
Hairuhusiwi kubeba pochi au mabegi katika jengo hili la mahakama isipokuwa kama yanaonyesha kilicho ndani au yanahitajika kimatibabu. Vitu vyovyote ambavyo ni muhimu kwa ajili ya shughuli za mtu mbele ya mahakama vinapaswa kubebwa kwa mikono au katika chombo cha wazi kinachoweza kukaguliwa kwa macho.
Kupata taarifa za mawasiliano za mahakama ya eneo lako au Kalani wa Mahakama ya Mzunguko, chagua wilaya yako kwenye menyu kunjuzi katika kisanduku cha buluu juu ya ukurasa huu (“Select a County”).
Wewe na Mkalimani wako wa Mahakama – Kujilinda wakati wa COVID-19
(PDF inayopakulika hapa)
Mahakama inakutaka wewe, mkalimani wako wa mahakama, na kila mtu aliye mahakamani kujilinda wakati wa dharura ya COVID-19.
Mkalimani wako ata:
- Atavalia barakoa (wakalimani wa lugha ya ishara hawahitajiki kuvaa barakoa)
- Kadri iwezekanavyo, adumishe umbali wa futi 6
- Atatafuta maeneo faragha ya kufasiri kwa ajili ya uwekaji mzuri wa umbali kati ya watu
- Atatumia vipokea sauti vya masikio au zana nyinginezo ili kufasiri kwa umbali ulio salama
- Kushirikiana na wafanyikazi wa mahakama ili kudumisha utakasaji wa vifaa
- Awe mwangalifu kuhusu kugusa makaratasi ambayo watu wengine wamegusa
Mkalimani wako HATA:
- Kusalimu kwa mkono
- Songea karibu nawe kwa ufasiri wa ufaragha zaidi
- Tumia kalamu au karatasi pamoja nawe
- Gusa simu yako ya mkononi/kifaa cha simu, hata kuangalia au kutafsiri ushahidi
Jinsi ya kujilinda ukiwa mahakamani:
YA KUFANYA:
- Nawa mikono yako mara kwa mara na sabuni na maji kwa angalau sekunde 20: Baada ya kupenga kamasi, kukohoa, kupiga chafya, au kutumia maliwato; na Kabla ya kula au kuandaa chakula cha kulisha mtoto
Usifanye HAYA:
- Kusalimiana kwa mkono, kugusa vitufe vya lifti, vishikio vya ngazi, au vitasa vya milango. Kutumia glavu au tishu kisha kutupa kiholela
- Ukigusa kitu chochote, usiguse uso wako - hasa macho, pua na mdomo wako - hadi utakapo nawa mikono yako
- Usiguse macho, pua na mdomo wako kwa mikono isiyosafishwa
Omba mahakama ipange upya tarehe yako ya mahakamani ikiwa:
- Una dalili au unapona kutokana na coronavirus, au
- Mtaalam wa afya alikuambia ujiweke katika karantini ya binafsi
Kwa taarifa kuhusu janga la COVID-19 tembelea:
Angalia kipengele cha Fomu, Machapisho, na Nyenzo hapo chini kwa ajili ya faharasa ya maneno ya kawaida ya sheria.